YA SINGO, MWESIGA na EDGAR
Katika kile kinachoonekana kama mwendelezo wa uchaguzi mkuu wa mnamo tarehe 31 october mwaka huu na madhara ya muendelezo huo, kumekuwa na matukio mbalimbali na mijadala lukuki kuhusu yaliyotokea katika uchaguzi huo, matokeo yake na baadhi ya matukio baada ya matokeo hayo, kwa mfano chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kususia hotuba ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kutoka nje ya bunge, baraza la mawaziri, spika na bunge n.k.
Thobias Mwesiga R, kama ilivyokuwa kwa watanzania wengi wapenda matukio na wadau wa maendeleo, hakuachwa nyuma na hayo yaliyokuwa yakiendelea katika nchi yake, nafsi yake haikupata faraja hadi pale alipoamua kutoa kile alichokiita “ maoni yake” kwa vyombo vya habari lakini hakuongelea kingine isipokuwa wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya bunge. Tarehe 19.11.2010. Akakutana na waandishi wa habari akisema yeye na wale aliowaita wanafunzi wa vyuo vikuu mkoa wa Dodoma, wanasikitiswa na kitendo kile kwa kuwa ni kinyume cha matarajio ya wapiga kura wa waheshimiwa hao. Akasema pia katika waraka wake au tamko lake hilo kuwa wanatekeleza maslahi yao bila kujali ya wapiga kura wao na kwamba huwezi kuacha kumtambua baba halafu ukatumia kila kinachotolewa na baba huyohuyo, akasisitiza tuwapuuze kwa kuwa ni wapotoshaji wakubwa, kwamba ni watovu wa nidhamu na tusikubali kudanganywa na watu wachache
Katika tamko lake hilo, ambalo nakala yake tunayo, Mwesiga na kile alichodai “kwa niaba ya vyuo vikuu mkoa wa DODOMA” anawataka wabunge hao waombe radhi kwa wapiga kura wa Tanzania, huku akisema lengo lao la sasa ni kuwachanganya watanzania.
Moja ya magazeti ya kila siku, likaripoti habari hiyo huku likisema wazi kuwa aliyejitambulisha kuwa waziri wa katiba na sheria wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ametamka kuwa wabunge waombe radhi.
Hiyo ikaifikia UDOSO, kwa kile kilichoonekana kuwa ni kuchukua hatua kali dhidi ya mwesiga, wakakanusha taarifa hiyo, na kuuomba uongozi wa social sciences and humanities kumchukulia “hatua kali”. Siku moja baada ya tamko hilo la UDOSO, mnamo tarehe 28.11.2010 tulishuhudia kile kilichokuwa na kichwa cha habari ‘TAARIFA KWA UMMA” ambamo mwenyekiti UDOSO (SSH) alitueleza kuwa bwana Thobias Mwesiga R, aliyekuwa akihudumu katika ofisi ya katiba na sheria, SI WAZIRI TENA katika wizara hiyo.
Siku mbili baadaye Bw. Thobias Mwesiga, aliomba kukutana na wanahabari wa UDOM akidai kuwa na “tamko lingine” kuhusu kuenguliwa kwake katika ‘kiti cha kuzunguka’ cha uwaziri.
Akiongozana na naibu wake(NASSA), katika mkutano huo alitueleza kuwa hakuwa na taarifa (hadi wakati huo) kuhusu kuondolewa kwake kuhudumu katika wizara ya katiba na sheria, akilonga kuwa hata yeye hana barua ya kuenguliwa kwake na kuwa “bado ni waziri” katika wizara hiyo, akasema kuwa hata yeye amesoma katika mbao za matangazo na kukuta barua kwenye ofisi ya spika na ile ya waziri mkuu.
Hata hivyo Mwesiga alimshutumu mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi (SSH)kuwa ametoa taarifa zinazokinzana akidai ameupotosha umma na wana ~udom kuwa yeye amefutwa kazi huku barua (ambayo nakala yake tuliiona) iliyopelekwa kwa waziri mkuu, spika, dean na DVC ikitamka kuwa amesimamishwa kazi.
Aliendelea kutupa makombora yake kwa mkuu huyo wa baraza la mawaziri la social sciences kuwa amakiuka makubaliano kati yake yeye na waziri mkuu Bw Edgar ya tarehe 2 juni 2010, yanayosisitiza kuwa katika kila jambo lihusulo UDOSO lazima waziri mkuu, makamu mwenyekiti, na mwenyekiti ahusishwe katika maamuzi na mwenyekiti Bw Leonard Singo alichukua maamuzi peke yake.
Alisema pia mwenyekiti hakufuata kanuni za baraza la mawaziri isemayo “ili hoja ipite lazima iungwe mkono na nusu ya baraza la mawaziri na huo ndio utakuwa msimamo wa baraza hilo . akaongeza pia kuwa Singo (Leonard) hakuunda kamati ya kuchunguza suala lake kama katiba inavyoagiza.
Alipoulizwa kuhusu taarifa yake kwa vyombo vya habari Mwesiga alisema “msimamo wangu ni ule ule na uko wazi” na kwamba alitumia uhuru wake wa maoni na mipaka ya uhuru huo kama ilivyoelekezwa na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania (Ib. 18, 20 na 30) huku akisisitiza kuwa chuo hakiongozwi na hisia za watu, kinaongozwa kwa kanuni na katiba.
Alipobanwa kwamba alitumwa na nani mwesiga alisisitiza “sikutumwa na mtu, nilichofanya ni kutoa mawazo yangu binafsi na ya wale tuliokuwa nao” na kwamba alilazimika kuwa “msemaji wao” kwa vile wasingeweza kuzungumza wote.
Akijibu swali la kwanini alisema “sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoa wa Dodoma ” Mwesiga alifafanua kuwa waliokuwepo walikuwa wana vyuo vikuu wa mkoa wa Dodoma na kwamba hakumaanisha wote. “kama unavyoona mwandishi hapo hakuna neno wote” alifafanua.
Tulipo hoji walikuwa wangapi na walikuwa wapi Mwesiga alisema kuwa walikuwa Dodoma Hotel na “kuhusu idadi siumbuki uizuri lakini almost kila chuo kilikuwa na mwakilishi” alisema akijibu swali la walikuwa wangapi.
Naye naibu waziri wa katiba na sheria hakuwa kimya kuzungumza juu ya suala hili kwani linaihusu wizara moja kwa moja naye alitoa mtazamo wake.
Naibu waziri anaanza kutoa maelezo ya kuwa suala lile kwa kuwa linamhusu waziri wa wizara ya katiba na sheria hivyo lilipaswa kufika kwenye wizara mapema ila suala la kufukuzwa bwana Mwesiga halikufika kwenye wizara na lilianzia kwenye mbao za matangazo
Naibu waziri aliendelea kufafanua ya kuwa waziri(Mwesiga) hakufukuzwa kwa kufuata misingi ya sheria (natural justice) ili aweze kutoa utetezi wake mbele ya vyombo husika
Naibu waziri anasisitiza kuwa mwenyekiti alitakiwa kutoa msimamo wa baraza la mawaziri na sio mtazamo wake mwenyewe. Hii ilienda sanjari na naibu waziri kutoa ufafanuzi wa kile kilichosemwa na bwana Singo kuwa Mwesiga amefanya ushabiki wa kisiasa, kwa kunukuu Ibara 51(a),(b),(c) ya sheria ya vyuo vikuu ya mwaka 2005.
1) No staff association or students' organization in an ition of
institution shall engage in any political party's activities on campus,
conduct its affairs or have a constitution which in any way or manner
whatsoever offends or conflicts with the provisions of this Act or of
any other written law.
political
parties
activities
on campus
(2) For the purpose of this section-
(a) ''campus'' includes any place where the activities or affairs
of the institution to which a staff association or a students'
organization belongs may under lease or licence take place,
be conducted or where the residence of students is
established, provided, organised or overseen whether
regularly or intermittently or on a particular occasion or
occasions;
(b) ''engaging in political parties activity'' includes regular
recruitment, training, registering or enrollment of political
party members, regular organisation of meetings, seminars
and conferences for a political party or political parties,
operating a branch office or cell or the like of a political
party or political parties and matters of a similar nature;
(c) ''staff association'' includes its members; and
(d) ''student organization'' includes its members.
Mwisho naibu waziri alisisitiza na kuwataka viongozi kufuata sheria katika kutoa maamuzi hata kama wamepewa mamlaka.
Suala hatukutaka liishie kwa Mwesiga bila kuathiri sheria za nchi hii tulipiga hodi kwa bwana Singo Leonard ili kupata ufafanuzi juu ya kile kilichoonekana ni kutofuata sheria
Singo anaanza kwa sisi kujua kuwa kuna tofauti kubwa kati ya makubaliano na mkataba, kwamba ndani ya makubaliano yake na Edgar Kihwelo yasiwe chanzo na sababu za malumbano yasiyo na msingi, huku akisisitiza kuwa serikali ya mseto ni kwa mataifa yenye dola na si kwa serikali za wanafunzi, pia kutoa ufafanuzi ya kuwa hakuna katiba ya mpito ya kuendesha kile kinachoitwa mkataba wa Singo na Edgar, viongozi wote wameapa kwa mujibu wa katiba na si kwa mujibu wa mkataba wa Edgar na Singo hivyo yeyote anayefanya jambo kinyume na taratibu za uongozi lazima achukuliwe hatua kali za kinidhamu. Pia akisisitiza kuwa Mwesiga hakuapa katika afisi ya waziri mkuu bali katika ofisi ya raisi.
Singo anasisitiza kuwa waziri amefanya makosa kwani nafasi za uongozi zinatambulika ndani ya chuo na si nje ya chuo hivyo Mwesiga hakupaswa kutumia dhamana ya watu waliompa yaani hakupaswa kutumia cheo chake cha waziri wa katiba na sheria nje ya chuo bila idhini ya wanachuo waliompa cheo hicho kwani cheo ni dhamana
Kama waziri, Mwesiga amesema uongo hivyo kudhalilisha jamii nzima ya wanaUDOM, kwani Mwesiga hajawahi kuwa msemaji wa wanavyuo vikuu wa mkoa wa Dodoma, pia hakuna umoja wa vyuo vikuu vya mkoa wa Dodoma kama upo aeleze ulianza lini na nani waanzilishi na nani viongozi wake, Mwesiga si waziri wa katiba na sheria chuo kikuu cha Dodoma bali katika chuo cha sanaa na lugha (kwa namna moja ama nyingine Mwesiga amevunja katiba ya Udoso Ibara ya 11f)
Singo anasisitiza kuwa katika mahafali ya chuo, Rais kikwete alitoa msisitizo kwa wanafunzi kujihusisha na masomo na siasa kuwaachia wanasiasa au pale mtu akihitimu ndipo aanze siasa, hivyo rais hakusema wanachuo wasijihusishe na siasa ndani ya chuo bali siasa kiujumla.
Singo anatufahamisha kuwa kikao cha Mwesiga na wenzake kilikuwa batili kwani UDOSO haikuwa na taarifa, hata wenzake kutoka vyuo vingine hawakutoa matamko kama alivyofanya yeye na kutoa msisitizoya kwamba waziri mkuu hana uwezo kikatiba kutengua uamuzi wa Rais kufanya hivyo tafsiri yake ni kejeli na kashfa kwa mamlaka ya rais
Singo anahitimisha kwa kusema kuwa mamlaka yake yanatoka kwa wananchi na kama hajatenda haki wananchi wapeleke malalamiko, mwisho anatoa msisitizo “sina muda wa kulumbana bali kushughulikia masuala kama field, afya, elimu kiujula, usafiri, usafi, sekta ya michezo pamoja na kufanya chuo kuheshimika ndani na nje.
Safari yetu ya kupata taarifa juu ya suala hili iliekea kwa waziri mkuu(SSH) bwana Edgar Kihwelo ambaye naye alitoa ufafanuzi na maelezo yake.
Bwana Edgar anadai kutofurahishwa na jinsi mfumo mzima ulivyotumika katika kulishughulikia suala “nyeti” kama hilo kwani halikuhitaji maamuzi ya haraka na mabavu kama ilivyotumika ilhali Serikali ya wanafunzi ina sheria na mamlaka yanayotambulika kisheria katika kushughulikia adhabu kwa makosa kama hayo. “Laiti kama mafisadi wangekuwa wanashughulikiwa na Raisi wa nchi bila kupitia mahakamani na mamlaka husika ili kuthibitishwa kama ni kweli wana hatia au la, basi kusingekuwa na umuhimu wa katiba na mamlaka zilizowekwa kwa mujibu wa katiba” Bwana Edgar aliongeza kwa msisitizo.
Alihitimisha kwa kutoa msimamo wake kuwa viongozi na wanafunzi kwa ujumla kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na mamlaka kabla, wakati na baada ya kufanya maamuzi. Pia aliwaasa viongozi wenzake kusoma na kuifuata katiba ya UDOSO ili kuondoa migogoro isiyokuwa na tija kwa jamii nzima ya wana UDOM.
HITIMISHO
Ndugu wana wa UDOM makala haya haya jaandaliwa kumsafisha mtu wala kumhukumu mtu, katika makala haya tumeandika kuhusu watu( SIngo, Edgar, Nassa na Mwesiga), tumejadili matukio na matokeo( tamko la mwesiga, wabunge wa chadema kutoka nje,waziri kusimamishwa, Waziri mkuu kupinga uamuzi wa rais) pamoja na masuala( waziri kuwajibishwa, kutii kanuni na taratibu)
Mambo ya kutafakari
1je!kulikuwa na ulazima wa Mwesiga kutoa tamko?
2.je! wapiga kura wa CHADEMA wanahitaji mtu wa kuwaambia eti wawapuuze wabunge wao?
3.je!Mwesiga aliwapa nafasi CHADEMA kuelezea kwa nini walitoka nje?(aliwafanyia natural justice)
4.je!ni kweli Mwesiga aliwasilisha mawazo yetu?
5.je! bunge la UDOSO linachukua vipi kitendo cha Singo kumuondoa katika uwaziri bwana Mwesiga?
6.Je! waziri mkuu alikuwa na sababu za kutumia lugha kali kukemea kitendo kilichofanywa na Mwenyekiti?
7.Je! viongozi wetu wamejifunza nini kuhusu tuio hili?
8.Je! nini mtazamo wa watu wa kawaida kwa wanachuo wa UDOM na wanavyuo wengine wa Dodoma ?
9. Je!matukio haya yametuletea heshima au fedheha kwa jamii?
10.Je! Singo atakuwa tayari kuomba msamaha endapo atabainika kuwa amefanya makosa kumuondoa Mwesiga katika nafasi ya uwaziri?
Makala haya yameandaliwa na Franklin Laurent(0712001954, 0759283880, frank.laurent@yahoo.com) Magooge Goodluck(0714061875, lucksonpromise@yahoo.com) na Reuben Gerald(0757463981, gnyaissa@yahoo.com) kwa kuzingatia
Katiba ya jamhuri, katiba ya udoso,student by laws na sheria ya vyuo vikuu ya mwaka 2005.{univesties act of 2005}
No comments:
Post a Comment