Tuesday, May 17, 2011

serengeti society katiba

                    CHUO KIKUU CHA DODOMA.
                            KATIBA YA KIKUNDI.

1.0    JINA LA KIKUNDI
Jina la kikundi litakuwa ni Serengeti Society of UDOM” (SSUDOM).
2.0    LUGHA ITAKAYOTUMIKA.
Lugha itakayotumika ni Kiswahili na/au kiingereza.
  3.0 MALENGO YA KIKUNDI.
       Lengo kuu la kikundi ni kuwaunganisha wanajamii wote wa wilaya ya      
       Serengeti walioko Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na;-
      i)Kusaidiana katika shida mbalimbali za kielimu na za kimaendeleo.
      ii)Kupongezana katika furaha mbalimbali.
    iii)Kuitisha vikao na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Serengeti kujadili            changamoto  mbalimbali za maendeleo ya wilaya.
    iv) Kushirikiana na vikundi mbalimbali vya kijamii vilivyoko nje na ndani ya chuo ili kuleta ufanisi katika maendeleo ya taifa.
4.0  DIRA NA DHAMIRA YA KIKUNDI.
i)Dira ya SSUDOM ni “Kukabiliana na changamoto za kijamii na kimaendeleo zinazoikabili jamii ya wana Serengeti walio chuo kikuu cha Dodoma na wilaya ya Serengeti kwa ujumla”
ii)Dhamira ya SSUDOM ni “SSUDOM ni umoja wa wanajamii wa Serengeti walioko UDOM waliojitolea kuleta maendeleo kwa wana Serengeti walio UDOM na wilaya kwa ujumla”
5.0      UANACHAMA.
1.      Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama wa SSUDOM kama atakuwa na sifa             zifuatazo
i)Awe ni mzaliwa na/au mkazi na/au mwenye asili ya wilaya ya Serengeti.
ii)Alipe kiingilio cha uanachama na michango yote inayomhusu kiasi kitakachopangwa na kikundi.
iii)Awe ni mwanachuo aliyedahiliwa katika chuo chochote (college) cha chuo kikuu cha Dodoma , au mwajiriwa aliyeajiriwa na chuo kikuu cha Dodoma.
2.      Mtu yeyote atakoma uanachama endapo lolote kati ya haya litatokea.
i)Atafariki dunia.
ii)Atajiudhuru uanachama kwa hiari yake mwenyewe.
iii)Mwanachama atashindwa kutimiza majukumu na wajibu wake kama mwanachama.
iv)Atafanya jambo lolote ambalo kama asingekuwa mwanachama angekosa sifa ya kuwa mwanachama.
6.0      HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA.
i)Mwanachama ana haki ya kutoa maoni yake katika vikao rasmi vya kikundi na   kusikilizwa .
ii)Mwanachama ana haki ya kuchagua na/au kuchaguliwa kuwa kiongozi wa kikundi.
iii)Mwanachama ana haki ya kuomba mkopo kutoka katika mfuko wa kikundi na anatakiwa kurudisha kwa masharti yatakayopangwa kikundi.
iv)Mwanachama anao wajibu wa kushiriki katika shughuli zote za kikundi zinazomhusu.
v)Mwanachama anao wajibu wa kuchanga kiasi kitakachopangwa na kikundi kwa ajili ya pongezi au kumfariji mwanachama atakayekuwa anastahili kupewa pongezi au faraja kwa mujibu wa kifungu cha 7 (1) katika katiba hii.
7.0      MICHANGO KWA WANACHAMA.
1. Bila kuathiri kifungu cha 6 (v) cha katiba hii, mwanachama atatakiwa kuchangia kiasi cha fedha kitakachopangwa na kikundi kwa mwanachama yeyote atakayepatwa na lolote kati ya haya.
i)Kufiwa na ndugu yake yeyote kati ya baba, mama, mke, mme, mtoto, baba mkwe, na mama mkwe.
ii)Mwanachama ataugua na kulazwa kwa muda kuanzia siku tatu mfululizo.
iii)Mwanachama ataoa au kuolewa.

2. Kikundi kitachangia kiasi kitakachopangwa na kamati kuu ya utendaji kutoka katika mfuko wa chama, kwa mwanachama yeyote atakayepatwa na lolote lililotajwa katika kifungu cha 7(1) cha katiba hii.
3.      Kikundi kitatoa zawadi kwa wanachama watakaohitimu kulingana na makubaliano ya kamati ya maandalizi ya kikundi kwa shughuli hiyo.
8.0      UONGOZI.
Kikundi kitakuwa na viongozi wafuatao.
8.1   MWENYEKITI.
Huyu ndiye atakuwa ndiye kiongozi mkuu wa kikundi na atakuwa na majukumu yafuatayo ;-
           i)Kusimamia mapato na matumizi ya kikundi
          ii)Kuongoza vikao vya kikundi kila inapohitajika.
          iii)Kupokea taarifa mbalimbali za wanachama.
8.2   KATIBU MKUU
 Huyu ndiye atakuwa ni mtendaji mkuu wa kikundi na atakuwa na majukumu yafuatayo.
          i)Kuitisha vikao vya kikundi kwa kukubaliana na mwenyekiti.
          ii)Kuandika na kutunza kumbukumbu za vikao.
         iii)Kuratibu shughuli za mapato na matumizi ya kikundi mbele ya wanachama.
         iv)Kutoa taarifa za maendeleo ya kikundi.
          v)Kutunza kumbukumbu na taarifa muhimu za wanachama wote.
8.3    KATIBU MKUU MSAIDIZI
                      i.            Huyu atakuwa ni msaidizi wa katibu mkuu katika shughuli zote za kikundi.
                    ii.            Katibu mkuu msaidizi atachaguliwa kutoka miongoni mwa naibu katibu mkuu wa College.
8.4    NAIBU KATIBU MKUU
i)Kutakuwa na Naibu katibu mkuu kutoka kila college isipokuwa kwa college itakayotoa katibu mkuu.
ii)Naibu katibu mkuu atakuwa na majukumu yote ya kikatiba katika ngazi ya college na atawajibika kwa katibu mkuu.
8.5    MTUNZA HAZINA.
Huyu atakuwa na majukumu yafuatayo.
i)Kutunza fedha za kikundi.
ii)Kuandaa taarifa za mapato na matumizi ya kikundi kila mwisho wa muhula          (semester)
8.6    MLEZI WA KIKUNDI
i)Kutakuwa na mlezi wa kikundi ambaye ndiye atakuwa mshauri wa kikundi kwa ajili ya maendeleo ya kikundi.
ii)Mlezi wa kikundi atatakiwa kuwa na sifa zote za kuwa mwanachama kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 5(1) cha katiba hii.
9.0      MUDA WA UONGOZI
i)Muda wa uongozi utakuwa ni mihula miwili ya masomo mfulululizo (mwaka mmoja wa masomo)
ii)Isipokuwa kwa mlezi ambaye atapatikana kwa kuteuliwa na kwa kuombwa kwa ridhaa yake, viongozi wengine wote watapatikana kwa njia ya kupigiwa kura.
10   MIKUTANO YA KIKUNDI.
i)Kutakuwa na mkutano mkuu wa kikundi kila jumapili ya mwisho wa mwezi na kila    panapokuwa na dharura.
ii)Wajumbe wa mkutano mkuu ni wanachama wote.
iii)Kutakuwa na mkutano wa kamati kuu ya utendaji kila mwezi ili kutathmini maendeleo ya kikundi.
iv)Wajumbe wa mkutano wa kamati kuu ya utendaji watakuwa ni mwenyekiti, katibu mkuu, katibu mkuu msaidizi, naibu katibu wakuu wa kila college, mtunza hazina na mjumbe mmoja (Neutral member) kutoka kila college.
v)Mwenyekiti wa kikundi ndiye atakuwa mwenyekiti wa mkutano mkuu na mkutano wa kamati ya utendaji.
vi)Katibu mkuu ndiye atakuwa katibu wa mkutano mkuu na mkutano wa kamati kuu ya utendaji.
vii)Katibu mkuu msaidizi atakaimu ukatibu wa vikao vya kikundi kama katibu mkuu hayupo.
11. VYANZO VYA MAPATO.
Kikundi kinategemea mapato kutoka kwenye vyanzo vifuatavyo kuendesha shughuli zake ;-
i)Ada ya kila muhula inayolipwa na wanachama.
ii)Misaada kutoka kwa watu binafsi, mashirika ya umma, mashirika binafsi n.k.
iii)Miradi mbalimbali itakayoanzishwa na kikundi.
12. UDHIBITI WA FEDHA ZA KIKUNDI
             i)Fedha zote za kikundi zitatunzwa benki katika akaunti ya kikundi.
ii)Fedha za kikundi hazitatolewa benki, isipokuwa kwa kuidhinishwa na waweka saini  (Signatories) watatu kati ya mtunza hazina, katibu mkuu, na wajumbe wawili (Neutral members) walioteuliwa na kamati kuu ya utendaji.
iii) Wajumbe wawili (Neutral members) waweka saini kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 12 ii) cha katiba hii watateuliwa na kamati kuu ya utendaji kutoka college tofauti na aliyotoka mtunza hazina na katibu mkuu.


                        ********************************

Dodoma,                                                                                 _________________  20/11/2010                                                                 Charles Ruge
                                                                                                 Mwenyekiti

No comments:

Post a Comment