CHUO KIKUU CHA DODOMA
SERENGETI SOCIETY OF UDOM (SSUDOM)
KANUNI ZA KIKUNDI KWA MWAKA 2010/2011
Kwa ajili ya kutoa tafsiri ya baadhi ya vifungu vya katiba ya SSUDOM, kanuni hizi zimetolewa ili kuendesha shughuli za kikundi kwa mwaka wa masomo 2010/2011
- Kila mwanachama atatakiwa kulipa kiingilio (Entrance fees) cha TSH 10,000/=
- Kila mwanachama atatakiwa kulipa Kiasi cha TSH 5,000/= kwa kila mhula isipokuwa kwa mhula aliolipia kiingilio.
- Kila mwanachama atatakiwa kutoa mchango wa TSH 3,000/= kwa ajili ya faraja au pongezi kwa mwanachama anayestahili kupewa kwa wakati huo.
- Kikundi kitatoa kiasi kitakachosalia kufika shilingi laki moja (100,000/=) kwa ajili ya faraja au pongezi kwa mwanachama anayestahili kwa wakati huo.
- Mkopo usiozidi shilingi laki moja (100,000/=) utatolewa kwa mwanachama atakayehitaji kufanya hivyo kulingana na mfuko wa chama.
- Mkopo kwa mwanachama hautakuwa na riba, ila mkopaji atatakiwa kulipa asilimia kumi (10%) kwa ajili ya gharama za kupata huduma za kibenki.
- Mwanachama atatakiwa kurudisha Kiasi cha fedha alichokopa kwa muda usiozidi miezi miwili.
- Mwanachama anayehitaji mkopo asiwe anadaiwa na kikundi wakati mkopo unapoombwa.
- Mapato na matumizi ya kikundi yatasomwa katika mkutano mkuu wa kila mwisho wa muhula.
NB Pesa ikishalipwa haitarejeshwa.
No comments:
Post a Comment